Jasmine Tridevil katika pozi.
MWANAMKE aliyejitambulisha
kwa jina la Jasmine Tridevil (siyo jina lake halisi) mwenye umri wa
miaka 21 amedai kufanyiwa upasuaji na kuongezwa titi la tatu kupitia
mahojiano aliyoyafanya redioni.
Jasmine ambaye ni raia
wa Tampa jijini Florida nchini Marekani anayejishughulisha na utoaji
huduma ya massage, alilipa kiasi cha dola za Kimarekani 20,000 sawa na
milioni 33.4 za Tanzania kufanyiwa upasuaji huo.
Mwanamama huyo katika
mahojiano na Real Radio 104.1 alidai kuwa ameamua kufanya hivyo ili
asiwe na mvuto kwa wanaume maana hataki kuwa na mpenzi huku akipenda
kuwa staa katika TV japo
alipoulizwa sababu ya kwa nini hataki kuwa na mwenza hakutaja sababu.
Takribani madaktari 50
walikataa kumfanyia upasuaji huo wakiogopa kuvunja miiko ya fani yao
hivyo kumchukua miaka miwili kumpata daktari aliyekuwa tayari kufanya
hivyo.
Kwa sasa mama huyo anarekodi video itakayoonesha changamoto anazokutana nazo akiwa mwanamke mwenye matiti matatu.
Mtaalam aliyemfanyia
upasuaji ambaye hakutaka kutajwa jina lake alichukua tishu katika tumbo
la mama huyo ili kutengeneza titi la tatu.
Jasmine amesambaza picha zake mpya akiwa katika vazi la bikini kupitia ukurasa wake wa Facebook baada ya upasuaji huo.
Mrembo huyo amedai kuwa amekanwa na mama yake mzazi pamoja na dada yake.
"Mama yangu alikimbia,
hataki kuongea na mimi wala hataki dada yangu aongee na mimi baada ya
kuongeza titi la tatu," Alisema Tridevil
Mbali na furaha
aliyonayo mrembo huyo, bado anadai titi lake la tatu halifanani na
mengine. Tridevil analazimika pia kujitengenezea mavazi yake mwenyewe
ambapo ananunua mavazi mawili ya kuogelea
kisha moja analikata ili kupata nguo itakayokaa kwenye titi lake la tatu.
0 comments:
Post a Comment