MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Richard Osward (40) mkazi wa
Tabata Segerea, hivi karibuni alinusurika kuuawa kwa kuchomwa moto na
wananchi baada ya kuhisiwa kuwa mwizi alipokutwa alfajiri akiwa na mfuko
ambao ndani yake kulikuwa na bomba, huko Segerea.
Richard Osward aliyechomwa moto na watu wenye hasira kali akidhaniwa
kuwa ni mwizi. Akizungumza kwa shida akiwa katika wodi namba 23 iliyomo
ndani ya Jengo la Sewa Haji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
Richard alisema tukio hilo lilimkuta akiwa ameongozana na rafiki yake
aliyemtaja kwa jina la Moses na kwamba walikuwa wakielekea Gerezani,
Kariakoo ambako wanajishughulisha na ufundi wa magari.
Akiuguza majeraha ya moto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Nilitoka nyumbani nikiwa nimebeba bomba katika mfuko nikitaka kwenda
kuliuza, tulipofika Segerea Seminari, tulisimamishwa na watu ambao
walitutilia shaka wakaanza kutupekua.
“Wakasema sisi ni wezi na hivyo lazima watuadhibu. Mara akapita
dereva wa bodaboda ambaye alishinikiza kuwa sisi ni wezi na kutaka
wachange hela wakanunue petroli ili watuchome moto, uzuri ni kwamba kwa
kuwa ilikuwa usiku,wakashindwa kupata hayo mafuta,
lakini tunashukuru dada mmoja alikuja amevaa sare za kampuni moja ya
ulinzi, akatukingia kifua na kusema watupeleke polisi na ndiyo
tukafikishwa Kituo cha Polisi cha Stakishari na baadaye kunileta hapa
kwa matibabu, kilichoniponza ni njaa lakini mimi ni mtu safi katika
jamii, mwenzangu alifanikiwa kukimbia.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment