Kesi ya jinai inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro imeahirishwa leo kwenye Mahakama Kuu Dar es Salaam hadi Septemba 22, mwaka huu.
Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Ponda anakabiliwa na mashtaka ya uchochezi kwenye maeneo mbalimbali mkoani humo, likiwamo la kukaidi amri ya Mahakama ya Kisutu iliyomtaka awe mhubiri amani katika jamii likiwa ni sharti la kifungo cha mwaka mmoja nje baada ya kumtia hatiani katika kesi ya jinai mwaka 2012.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment