AMA kweli fedha mwanaharamu! Kama bado
ulikuwa ukiamini kwamba Beautiful Onyinye,
Wema Isaac Sepetu anayependelea kuitwa
Madam ana mtonyo (fedha) kumzidi aliyekuwa
shosti wake, mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’,
umekosea sana kwani upepo umegeuka.
Habari za ‘ufukunyuku’ zinadai kwamba, kwa
utajiri alionao kwa sasa, Kajala anaweza
kudiriki kumwajiri Wema kama kisemavyo
chanzo.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na wote
kwa maana ya kutafuna pande zote, mwigizaji
huyo ambaye enzi za ushosti wake na Wema
alikuwa akionekana kama kijakazi, sasa fedha
imemtembelea kiasi cha kutosha wakati
mwenzake kwa bahati mbaya eti ‘anatembelea
ringi’.
Chanzo kilisema kwamba Kajala kwa sasa ana
maisha ya ‘kitonga’, amepanga kwenye nyumba
nzuri ya ghorofa, ana kampuni yake ya filamu
(KAY Entertainment), magari manne,
anatembea na wapambe (walinzi) huku akaunti
yake benki ikiwa imetuna.
Nyota wa muvi za Kibongo, Kajala Masanja Akiwa
na WEMA
“Kajala ameonesha jeuri ya fedha.
Ametoka katika nyumba ya kawaida sasa
analala angani. Kwa taarifa yenu
amepanga ghorofa nzima maeneo ya
Sinza-Madukani jijini Dar.
“Yupo vizuri, anamiliki ofisi kubwa ya
kuzalisha sinema, magari mawili ya ofisi
pamoja na magari mawili ya kutembelea
(Brevis na Harrier) na anaishi katika nyumba
anayolipa kodi kwa mwezi dola 2,000 (zaidi ya
Sh. milioni 3.2),” kilidai chanzo hicho na kudai
kwamba si mbaya Kajala akamkumbuka
mwenzake hata kwa kumwajiri kwenye
kampuni yake.
KAJALA AMEHONGWA?
Akizungumza na waandishi wetu, Kajala
alisema anamshukuru Mungu kwani fedha hizo
amezizalisha kupitia kazi zake pamoja na
biashara mbalimbali alizokuwa akizifanya,
hajahongwa na mtu yeyote.
“Sijahongwa na mtu yeyote, kila mtu ana akili
zake katika kutafuta fedha, nafanya biashara
huku nikiigiza sinema zangu na Mungu
amenijalia mambo yanakwenda vizuri,” alisema
Kajala.
Kuhusu kumwajiri staa mwezake huyo, Kajala
hakutaka kulizungumzia hilo.
WEMA HALI IPOJE?
Utafiti uliofanywa na Ijumaa Wikienda
umebaini kwamba Wema aliyemlipia Kajala Sh.
milioni 13 asiende jela mwaka jana, ambaye
kipindi kifupi kilichopita alikuwa na kampuni
ya kuzalisha sinema, wapambe, akaunti
iliyonona benki, magari ya kifahari ya
kutembelea na samani nyingine, nyingi
zimepotea kama si kuyeyuka kabisa.
Gari la aina ya Toyota Brevis inayomilikiwa
na Kajala.
Utafiti umeonesha Wema ambaye alikuwa
akimiliki magari kadhaa likiwemo la kufanyia
kazi za sinema, kwa sasa amebakiwa na gari
moja tu ambalo ni Toyota Harrier.
Kama hiyo haitoshi, ilidaiwa kuwa hata akaunti
benki haijanona na hata wapambe wa
kutembea naye wameyeyuka.
WEMA ATAFUTWA
Ili kutaka kujua anazungumziaje ‘challenge’
hiyo ya kudaiwa kuporomoka kiuchumi,
wanahabari wetu walimtafuta Wema kwa siku
tatu mfululizo lakini hakupatikana huku simu
yake ikiita muda mrefu bila kupokelewa.
SHOSTI WAKE
Akizungumza na waandishi wetu kwa sharti la
kutoanika jina , rafiki wa karibu wa Wema
alikiri kuwa staa huyo mwenye nyota
isiyochuja, ameshuka kiuchumi tofauti na enzi
zile ambazo walikuwa wakitanua katika viunga
mbalimbali na msururu wa watu huku Madam
akisimamia shoo nzima ya malipo.
“Madam kwa sasa ameshuka kiuchumi kwani
hatutanui mjini kama ilivyokuwa zamani,
yaani naamini anaweza kuajiriwa na Kajala
ambaye wakati ule alikuwa chini kwake,”
alisema rafiki huyo.
KUMBUKUMBU YA JUZIKATI
Hivi karibuni, baadhi ya mashabiki wa Wema
ambao wanajiita Team Wema, walimuonya staa
wao huyo wakidai ananyonywa na mpenzi
wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
ambaye pia amekuwa akimdhalilisha katika
majukwaa pindi anapofanya shoo zake.
Walimtaka abadilike kwani yeye ndiye mwenye
nyota ya kung’aa lakini Diamond ananufaika
yeye peke yake na muziki wake.
DIAMOND ALINENA
Baada ya Diamond kushambuliwa na Team
Wema, naye alitoa majibu ambayo yalionesha
dhahiri kwamba ndiyo sababu inayomfanya
Wema ashuke kisanaa na kiuchumi.
“Kama kweli mnampenda huyo msanii
wenu (Wema) basi mngemshauri kwanza
akaacha kufanya starehe kuliko kuelekeza
lawama kwangu, mimi kama mume,
jukumu langu ni kuhakikisha namwezesha
kuanzisha biashara lakini jukumu la
kuendeleza ni la kwake, mnataka hata
kuigiza nikamuigizie?,” alihoji Diamond
mtandaoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment