Stori: Ojuku Abraham
HAKUNA lugha nyingine ya kusema zaidi ya kuainisha kuwa pepo wa ajali za barabarani zinazoua mamia ya watu ni uzembe wa kutisha unaofanywa na madereva katika uendeshaji magari bila utii wa sheria. Basi la Mtei Express likiovateki wakati kuna magari mawili yanakuja kwa mbele.
HAKUNA lugha nyingine ya kusema zaidi ya kuainisha kuwa pepo wa ajali za barabarani zinazoua mamia ya watu ni uzembe wa kutisha unaofanywa na madereva katika uendeshaji magari bila utii wa sheria. Basi la Mtei Express likiovateki wakati kuna magari mawili yanakuja kwa mbele.
Uchunguzi wa Gazeti la Ijumaa uliofanywa hivi karibuni katika maeneo
mbalimbali nchini umebaini kuwa, mbali na mwendo kasi unaotajwa mara kwa
mara kuwa unachangia ajali, suala la kutozingatia sheria za usalama
barabarani ni hatari zaidi.
Picha za magari ya abiria yaendayo mikoani zilizotumika ukurasa wa nyuma
wa gazeti hili ni kielelezo tosha kuwa madereva wengi hawajui sheria za
usalama barabarani au wanazivunja makusudi jambo ambalo husababisha
kutokea kwa ajali nyingi za magari kugongana uso kwa uso.
Katika ajali kubwa na mbaya iliyotokea wiki iliyopita mjini Musoma na
kuua zaidi ya watu 40, ilitokana na mabasi mawili ya J4 na Mwanza Coach
kugongana uso kwa uso katikati ya daraja; kukosa umakini kwa madereva ni
chanzo.
Uamuzi wa kizembe kama huo na ule unaonekana katika picha zilizobeba
habari hii ambapo madereva wa magari husika wanaonekana ‘kuovateki’
kinyume cha muongozo wa uendeshaji.Sheria zinamkataza dereva kulipita
gari jingine kwenye mlima, mteremko mkali na mahali penye kona, lakini
kwa mshangao madereva wengi wamekuwa hawazingatii hilo.
“Ukisafiri hasa kwenye barabara kubwa kuna alama zinazokuongoza, lazima
dereva uzifuate, lakini madereva wetu hawafanyi hivyo, inawezekana
hawajui sheria au wanapuuza kwa sababu adhabu zetu ni nyepesi tofauti na
nchi nyingine kama Rwanda,” alisema Mohammed Mpinga, Kamanda wa Kikosi
cha Usalama Barabarani nchini katika mahojiano na gazeti hili hivi
karibuni.
Hata
hivyo, mbali na uvunjifu huo wa sheria, uchunguzi wetu umebaini kwamba
madereva wengi wamekuwa wakiendesha magari huku wakiwa wamelewa pombe na
hivyo kuwafanya wakose umakini.
Mbali na ulevi baadhi ya madereva wa mabasi yaendayo mkoani wamekuwa
wakiendesha kwa mashindano ya kuwahi kufika waendeko ili wasifiwe na
abiria kuwa wamewawahisha jambo ambalo mwishowe kuwahi huko huwatokea
puani na kuwasababishia ajali.Taarifa ya polisi inaonesha kwamba kwa
mwaka jana pekee kulikuwa na ajali 23,842, kati ya hizo ni za mabasi
931, zilizoua watu 313.
0 comments:
Post a Comment