Naibu
katibu mkuu wa wizara ya habari ,utamaduni na michezo Profesa Elisante
Ole Gabriel akimkabidhi kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars 2014
nahodha wa timu ya wasichana ya Temeke Fatuma Issa baada ya kuibuka
mabingwa. naeshudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil
Colaso.
Makamu
mwnyekiti wa chama cha soka cha wanawake Tanzania Rose Kisiwa
akimkabidhi kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars 2014 nahodha wa timu
ya mkoa wa kisoka Kinondoni Fred Mazuri Baada ya kuibamiza Ilala 5 –
3, Jumapili jijini Dar-es-Salaam.
Wachezaji
wa timu ya mkoa wa kisoka ya Kinondoni wakishangilia ubingwa wa Airtel
Rising Stars 2014 baada ya kuifunga timu ya Ilala 5 – 3, Jumapili jijini
Dar-es-Salaam.
Timu
ya Kinondoni wavulana imetwaa uchampioni wa mashindano ya vijana chini
ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars kwa kuifunga timu ngumu ya
Ilala 4-2 kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya sare ya 1-1
katika muda wa kawaida wa dakika 90.
Mechi
hiyo iliyotanguliwa na shamra shamra za maandamano na halaiki, ilikuwa
yenye upinzani mkali na baada ya kosa kosa za hapo na pale Kinondoni
walipata goli katika dakika ya 31 kupitia kwa Kassim Kitwana kwa shuti
kali la mbali lililomshinda mlinda mlango wa Ilala Sulum Siasa.
Goli
hili lilibadili kasi ya mchezo huku Ilala wakitafuta goli la
kusawazisha na juhudi zao zilifanikiwa kuzaa matunda katika dakika ya 40
baada ya kutoke piga ni kupege golini mwa timu ya Kinondoni na mchezaji
hatari Juma Yusufu kufunga kwa huti la karibu.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kushambuliamba kwa zamu lakini hakuna timu
iliyofanikiwa kupata goli la kuongoza hadi dakika ya mwisho. Ndipo refa
akaamua kumaliza ubishi kwa penati.Katika penati tano, Kinondoni
walifunga kupitia kwa Abdul Malangali, Milaji Gwangaya, Omri Rashid na
Abubakari Nuru wakati Kassim Kitwana alipaisha. Kwa upande wa Ilala
waliofanikiwa kufunga ni Abdul Bitebo na Rashid Mohamed wakati Maisala
Adam na nahodha wa timu Shaban Zuberi walikosa.
Akifunga
fainali hizo za taifa za Airtel Rising Stars, mgeni rasmi Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Professor
Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Naibu Waziri wa wizara hiyo Mheshimiwa
Juma Nkamia, aliipengeza kampuni ya Airtel kwa kujitokeza kusaidia
maendeleo ya soka hapa nchini.
Alitoa
wito kwa vijana kuzingatia nidhamu katika michezo na kujituma ili
kupata mafanikio na kusema kuwa katika dunia ya leo soka ni chanzo cha
ajira kwa vijana wengi. Pia alisema kuwa kufanikiwa kwao kutaiwezesha
Tanzania kufahamika zaidi kimataifa. Naye Mkurungenzi Mtendaji wa Airtel
Tanzania Sunil Colaso amesisitiza nia thabiti ya kampuni yake kuendelea
kudhamini mashindano ya vijana ya Airtel Risig Stars.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment