Mpoto ameiambia jaka the swaga blog kuwa amesemwa sana kuhusu tabia ya kuto vaa viatu lakini ameshindwa kubadilika.
“Beauty yoyote ipo kwenye jicho,unapozungumzi Mrisho Mpoto kuwa peku ,sehemu nyingi sana,mara nyingi sana watu wananiona peku, ni kwa sababu ya kutafuta energy ,unajua energy ya mimi kuendelea kuishi inapatikana kwenye udongo,yani ngozi yangu inapokutana na ardhi nakuwa so (confident) na nakuwa Mpoto, zaidi na nguvu na nakuwa na akili ,sasa sipendi wakati mwingine kuwa fake,najitaidi sana kuwa wakisasa ila nakuwa nasahau,kwamfano naweza nikanunu kiatu cha gharama alafu nikakisahau kwenye ndege au kwenye basi kwasababu siyo kawaida yangu kuvaa viatu, nisha jaribu lakini nimeshapoteza vingi,kwasababu siyo culture yangu kuvaa viatu ,viatu navaaga kwasababu watu wananisema.kwaiyo nikivaa ninakuwa kama inanisumbua, nikaona kama bora niache,alafu nakuwa siko huru,ukinikuta nimevaa viatu alafu tukaanza kufanya mazungumzo nakuwa siko huru kwasababu nakuwa nipo kama naelea hewani,yani kama sina chaji,kwaiyo kwangu mimi ardhi ni kama plug ya mwili wangu,nikikanyaga chini wewe niulize chochote nitakujibu niambie niandike shairi la haina yoyote,mimi ata nikiandika nyumbani kwangu lazima niweke miguu kwenye mchanga,ata nyumbani kwangu hakuna mchanga mimi ninabeseni kabisa la michanga,kwajili tu yakukanyaga yani nikiandika nakuwa confidant ata nikiandika

nakuwa na amani”Alisema Mpoto
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO

0 comments:

Post a Comment

BURUDANI

 
Top